Klabu ya Bayern Munich imetoa hasira zake hapo jana katika mchezo wa Bundesliga wa raundi ya 8 baada ya kuichapa Bayer Leverkusen kwa mabao 4-0 wakiwa nyumbani kwao Allianz Arena.

 

Bayern Amaliza Hasira Zake kwa Leverkusen

Mabao hayo yalitupiwa katika vipindi tofauti, ambapo kipindi cha kwanza yaliwekwa mabao matatu, na kipindi cha pili lilifungwa bao moja. Ambapo Leroy Sane, Jmal Musiala, Sadio Mane na Thomas Mane ndio wafungaji wa mabao hayo yaliyoipa Bayern ushindi.

Bayern ilipata alama tatu hapo jana baada ya kuzikosa takribani mechi nne kwenye ligi kuu ya Ujerumani. Matokeo hayo yalifanya Klabu hiyo kuanza kuchanganyikiwa lakini jana mambo yakawa vizuri.

 

Bayern Amaliza Hasira Zake kwa Leverkusen

Julian Nagelsman afurahia timu yake kurejea kwenye hali yake ya zamani ya kupata matokeo ya kuridhisha. Matokeo hayo yameifanya timu hiyo kupanda hadi nafasi ya pili huku akisubiria matokeo ya timu nyingine.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa