Klabu ya Fc Bayern Munich inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga imeendelea kua na matokeo ya kutoridhisha katika ligi hiyo.

Mabingwa hao watetezi wamekua na kiwango kibovu kwenye ligi hiyo kwenye michezo takribani minne ya mwisho waliocheza katika ligi hiyo na kupata matokeo ambayo sio ya kuridhisha kwa wanabavarian hao.

bayern munichKlabu hiyo leo imedondosha alama tatu katika mchezo waliokuepo ugenini dhidi ya klabu ya Augsburg kwa bao moja kwa bila lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Berisha mnamo dakika ya 59 ya mchezo katika kipindi cha pili na likadumu mpaka kumalizika kwa mchezo na kuacha alama zote tatu katika dimba la WWK Arena.

Bayern Munich wamedodosha alama tisa katika michezo yao minne ya nwisho baada ya kusuluhu michezo mitatu kabla ya kufungwa mchezo wa dhidi ya klabu ya Augsburg kitu kinachoonesha ishara mbaya kwenye timu hiyo klabu hiyo kutoka kuongoza msimamo wiki kadhaa mpaka kushuka nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa