Klabu ya Bayern Munich inakaribia kumnasa kiungo wa klabu ya Rb Leipzig Konrad Laimer katika majira ya joto mwezi juni 2023.
Bayern Munich watampata kiungo huyo kwa usajili huru kwani mchezaji huyo atakua amemaliza mkataba wake na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani,Klabu Fc Bayern imekua na ushawishi mkubwa katika soka la Ujerumani na wamekua wakipata wepesi wanapohitaji mchezaji yeyote kwenye timu yeyote ndani ya ligi hiyo.
Bayern Munich inaelezwa wako katika nafasi nzuri zaidi ya kumsajili mchezaji huyo mwishoni mwa msimun huu kwani wamekua na mazungumzo na mchezaji huyo kwa muda sasa, Na kocha wa klabu hiyo Julen Nagelsman amekua akivutiwa na mchezaji huyo na kumuhitaji kuungana nae kwa miamba hiyo ya soka nchini Ujermani.
Kiungo Konrad Laimer anahitaji kucheza klabu ya Fc Bayern katika na anaonesha kuvutiwa na timu hiyo toka mwaka 2021 majira ya joto ila mazungumzo hayakwenda vizuri baina ya klabu yake na Bayern kitu kilichosababisha dili hilo kutokamilika.