Klabu ya Bayern Munich imetaarifiwa kutuma ofa kwa klabu ya Tottenham kwajili ya kupata huduma ya mshambuliaji wa klabu hiyo nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane.
Bayern Munich wametuma ofa ya kiasi cha Euro milioni 70 leo kwa klabu ya Tottenham kwajili ya mshambuliaji Harry Kane, Vyanzo mbalimbali vimeripoti kua mabingwa hao wa soka nchini Ujerumani wanamuhitaji mshambuliaji huyo sana.Harry Kane amekua kama dhahabu sokoni msimu huu kwani amekua akifuatiliwa kwa karibu na vilabu kadhaa barani Ulaya, Manchester United wanatajwa kumfatilia kwa kiwango kikubwa lakini klabu yake bado inaonesha ugumu kumuachia.
Bayern Munich inafahamika wana shida ya mshambuliaji na hawajafanikiwa kupata mshambuliaji mwenye kiwango cha dunia tangu Roberto Lewandowski alipoondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita.Klabu ya Tottenham inataarifiwa inataka kiasi cha paundi milioni 100 ili kumuachia Harry Kane, Huku Bayern Munich mpaka sasa wakiwa wametuma kiasi cha Euro milioni 70 hivo hii inaonesha bado kutakua na usumbufu kutokana na bei hiyo waliyoitoa.