Bayern Munich Wamtolea Macho Rangnick

Klabu ya Bayern Munich ipo kwenye mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya Austria raia wa kimataifa wa Ujerumani kwajili ya kuifundisha klabu hiyo msimu ujao.

Bayern Munich itakua haina kocha mwishoni mwa msimu kwani kocha wake wasasa Thomas Tuchel ataondoka klabuni hapo baada ya msimu kumalizika, Hivo klabu hiyo ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya kuelekea msimu ujao.bayern munichKocha Rangnick ambaye amewahi kuifundisha klabu ya Man United ameanza mazungumzo na miamba hiyo ya soka nchini Ujerumani ili kuangalia uwezekano wa kuweza kuinoa timu hiyo msimu ujao.

Mazungumzo yanaendelea kwa pande zote mbili na inaelezwa mazungumzo yamefikia hatua nzuri baina ya kocha huyo na klabu hiyo, Hivo Rangnick yupo kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuchukua nafasi ya kocha Thomas Tuchel.bayern munichSuala mshahara ndani ya klabu ya Bayern Munich sio jambo kubwa sana kwa kocha Rangnick, Huku yeye akilenga zaidi kujua mpango wa muda mrefu wa klabu hiyo lakini pia kua na maamuzi kwenye usajili wa wachezaji wanaoingia na wanaotoka.

Acha ujumbe