Bayern Munich tayari wamepanga bei yao kwa Robert Lewandowski, hii ni kwa mujibu wa Kicker kupitia Mundo Deportivo.

Wanadai kuwa klabu hiyo ya Bavaria inataka ada isiyopungua €40m kwa mshambuliaji wao wa thamani kutoka Poland.

Lewandowski, 33, ana mkataba na Bayern unaofikia msimu wa joto wa 2023 na msimamo rasmi wa kilabu ni kwamba atakamilisha mkataba wake na wanafanyia kazi suala la kuuongeza zaidi.

Suala la mkataba mpya linaweza kuwa changamoto. Bayern wanachelewa kuongeza kandarasi za wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30 kwa zaidi ya miaka miwili.

Kwa kuzingatia hilo Barcelona wamehusishwa na uhamisho wa staa huyu.

La Blaugrana wana nia ya kumpata nambari tisa wa kiwango cha juu baada ya kushindwa kumpata Erling Haaland wanaweza kwenda kwa Lewandowski. Suala la kuweza kumudu gharama linaweza kuwa ni suala jingine.

Staa huyu amekuwa bora, na ni mmoja wa washambuliaji hatari katika soka la Uropa, Lewandowski amefunga mabao 47 katika mechi 42 kwenye mashindano yote akiwa na Bayern msimu huu.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa