Beckham Atimiza Miaka 30 Tangu Acheze Mchezo wa kwanza United.

David Beckham leo ametimiza miaka 30 tangu acheze mchezo wake wa ndani ya klabu ya Manchester United ikiwa na maana Becks alicheza mchezo wake wa kwanza tarehe kama ya leo mwezi tisa mwaka 1992.

Beckham ni mchezaji ambae amekuzwa katika shule ya vijana ya klabu hiyo kabla ya kupata nafasi ya kucheza timu ya wakubwa ya Manchester United ambapo alipata mafanikio mengi na timu na kua miongoni mwa magwiji wanaokumbukwa katika timu hiyo yenye wapenzi wengi duniani.

bekhamStaa huyo wa kiingereza alifanikiwa kucheza michezo 265 ya ligi kuu ya Uingereza na kufanikiwa kufunga mabao 61 huku akicheza michezo 81 ya ligi ya mabingwa barani ulaya na kufunga mabao 15,Becks amefanikiwa kushinda mataji sita ya ligi kuu ya Uingereza na klabu hiyo,mataji mawili ya Fa pamoja na taji moja la ligi ya mabingwa ulaya.

Nyota huyo alifanikiwa kudumu katika timu hiyo kwa miaka 12 kabla ya kutimkia klabu ya Real Masrid mwaka 2003 ambapo pia alikwenda kucheza kwa mafanikio makubwa.

Staa huyo atakumbukwa zaidi kama fundi wa mipira iliyokufa wakati anacheza haswa katika ligi kuu ya Uingereza ambapo anaongoza kufunga magoli ya mipira iliyokufa akiwa na magoli 18 akifuatiwa na James Ward Prowse mwenye mabao 14.

Beckham anabaki kama gwiji wa klabu hiyo zaidi wanapewa heshima kama kizazi bora cha mwaka 1992 akiwa na wenzake kama Paul Scholes,Garry Neville,Phil Neville,pamoja Nicky Butt.

Acha ujumbe