Moja wa beki muhimu aliyejitengenezea utawala wake Hector Bellerin ameripotiwa kuwa amewaambia mabosi wa Arsenal kuwa anatamani kwenda kukipiga katika mabingwa wa Serie A, Inter Milan.

Japo hakuna dili rasmi lililopelekwa Arsenal na Inter Milan kuhusu kuhitaji saini ya mchezaji huyo, lakini ni ukweli kuwa Bellerin ni moja ya majina yaliyotajwa kuwa katika shabaha za Inter Milan kufuatia kuondoka kwa Achraf Hakimi kwenda PSG kwa dau la Euro Milion 60.

Washika bunduki hao wa London wapo tayari kuachana na nyota huyo ambaye anacheza kama beki wa kulia hata kwa mkopo kwa sharti la kuuzwa moja kwa moja kutokana na uchezaji wake.

Bellerin alijiunga na Arsenal akitokea akademi ya Barcelona mnamo mwaka 2011 na mpaka sasa amecheza mechi 239 na kujishindia mataji matatu ya FA na makombe matatu ya ngao ya jamii.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa