Bellingham Kukipiga dhidi ya Uswisi Licha ya Kufungiwa

Kiungo wa kimataifa wa Uingereza Jude Bellingham na klabu ya Real Madrid Jude Bellingham atacheza mchezo wa robo fainali wa michuano ya Euro 2024 dhidi ya Uswisi licha ya kufungiwa.

Bellingham amefungiwa pamoja na kupigwa faini na shirikisho la soka barani ulaya Uefa baada ya kuonekena  kushangilia kwa namna ambayo imetafsiriwa kama kejeli kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Slovenia katika mchezo wa hatua ya 16 bora.bellinghamKiungo amefungiwa mchezo mmoja na faini ya €30 ambayo atatakiwa kulipa lakini mchezo mmoja ambao amefungiwa kiungo huyo wa klabu ya Real Madrid hautamnyima kucheza mchezo wa robo fainali dhidi ya Uswisi, Kwani adhabu hiyo itadumu ndani ya mwaka mmoja hivo anaweza kuchagua mchezo wa kutokucheza ndani ya mwaka mmoja.

Baada ya Bellingham kufungiwa na kuweza kupata fursa ya kucheza imeibua taharuki kwani beki wa kimataifa wa Uturuki Merih Demiral yeye amefungiwa mchezo mmoja pia, Lakini yeye hataweza kucheza mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi.

Acha ujumbe