Beki wa kulia wa kimataifa wa Uingereza ambaye anakipiga ndani ya klabu ya Arsenal Ben White inaelezwa yupo kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na washika mitutu hao wa London.

Mchezaji Ben White yupo kwenye hatua nzuri ya kuongeza kandarasi ya kuendelea kuitumikia klabu ya Arsenal kwa muda mrefu, Kwani mazungumzo mpaka sasa yanaendelea vizuri.Ben whiteKocha Mikel Arteta akiongelea suala la beki huyo kuongeza mkataba mpya alisema “Kila siku tunajitahidi kuiweka klabu kwenye mazingira salama kwa namna yeyote na Edu pamoja na klabu wanalifanyia kazi suala hilo”

Taarifa zinaeleza kua mpaka sasa mazungumzo yapo kwenye hatua nzuri na upande wa klabu na mchezaji wote wamekubaliana, Hivo ni mambo machache yamebakia ili kukamilisha mchakato huo na beki huyo kusaini dili jipya klabuni hapo.Ben whiteBeki Ben White alijiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2021 na kufanikiwa kua moja ya wachezaji muhimu klabuni hapo mpaka sasa, Ikiwa ndio sababu ya Arsenal kuhitaji kumuongezea mkataba mpya juu ya awali ambao unamalizika mwaka 2026.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa