Benjamin Pavard Aingia Rada za Ten Hag

Beki wa klabu ya Fc Bayern Munich Benjamin Pavard raia wa kimataifa wa Ufaransa ameingia kwenye rada za kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag.

Benjamin Pavard inaelezwa yupo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanahitajika kwenye nafasi ya ulinzi na kocha wa klabu ya Man United, Huku mpaka sasa hakuna ofa yeyote iliyotumwa kuelekea klabu ya Bayern Munich.Benjamin PavardMan United mpaka sasa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumuachia beki wake raia wa kimataifa wa Uingereza kuelekea klabu ya West Ham, Hivo watahitaji beki mwingine wa katikati kwajili ya kuziba nafasi ya mchezaji huyo.

Taarifa zinaeleza kocha Erik Ten Hag amemfukuzia beki huyo kwa miezi kadhaa nyuma na ameshaueleza uongozi kua beki huyo ni moja ya mabeki anaowahitaji, Hivo suala hilo bodi ya usajili kwasasa ndio inalifatilia kwakua kocha huyo ameshapendekeza na ameachia uongozi.Benjamin PavardMbali na beki Benjamin Pavard Man United pia inaelezwa kuwafatilia mabeki wengine kama Edmond Tapsoba anayekipiga katika klabu ya Bayern Leverkusen na Jean Todibo anayekipga klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa.

Acha ujumbe