Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema anatarajiwa kuanza katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Liverpool utakaopigwa katika dimba la Anfield.

Karim Benzema alikosekana katika mchezo wa Real Madrid waliopata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya klabu ya Osasuna katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania, Sababu za kukosekana katika mchezo huo zilielezwa ni kwajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Liverpool ambao utapigwa mapema.benzemaKlabu ya Real Madrid leo watapambana na klabu ya Liverpool katika dimba la Anfield ambapo klabu ya Liverpool itakua nyumbani ikiangalia namna inavyoweza kulipa kisasi dhidi ya mabingwa hao watetezi wa ulaya ambao walichukua ubingwa mbele ya Liverpoo.

Kocha Carlo Ancelotti licha ya Benzema kutarajiwa kuanza katika mchezo w aleo dhidi ya Liverpool anaamini Vinicius ataendelea kuwasha moto katika mchezo huo, Vinicius alikua na kiwango bora sana katiika mchezo wa wikiendi dhidi ya klabu ya Osasuna.benzemaKocha Ancelotti anafurahia kurejea kwa Benzema kwenye kikosi chake huku akiwa na matumaini na kikosi chake kuelekea mchezo wao dhidi ya Liverpool usiku wa leo, Kocha huyo anasema licha ya kukosekana kwa Kroos na Tchouameni lakini kikosi kinaonekana kiko vizuri kwasababu waliochukua nafasi zao wanafanya vizuri.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa