Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelloti amesema kuwa anatarajia mshambuliaji wake Kareem Benzema anaweza kurejea kwenye mechi ya Dabi kati yao na Atletico ambayo inatarajiwa kupigwa Septemba 18 ambapo atazikosa mechi zijazo za ligi ambazo ni dhidi ya Marlloca na RB Leipzig kimataifa.
Benzema alitoka nje na jeraha la goti wakati Madrid iliposhinda 3-0 dhdi ya Celtic katika mchexzo wa ufunguzi wa makundi wa ligi ya mabingwa Ulaya Jumanne na alihofiwa kwamba angekosa kipindi muhimu kutokana na matokeo muhimu.
Hata hivyo Ancelloti alionekana kuondoa hofu kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumamosi kabla ya mchezo wa Los Blancos dhidi ya Real Mallorca, akisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kurejea baada ya wiki moja. Na baada ya mechi hiyo watakipiga dhidi ya RB Leipzig kwenye michuano ya klabu bingwa kabla ya kumenyana na Atletico Madrid.
Kocha aliongezea kwa kusema hatutamlazimisha Benzema, Hakika hatacheza kwenye mechi ya Leipzig lakini kwenye dabi atakuepo lakini pia alisema sitarajii Hazard acheze kama Benzema, lakini nataka acheze vizuri na kuungana na washambuliaji wengine.