Bernard Morrison Usiposikia La Mkuu, Mimi Simo

Asante kidogo kwa Flyover za Ubungo, kidogo mpaka walala hoi tunapaa juu kama ndege na foleni imekatika kidogo na pongezi tena Tazara kwa Injinia Mfugale watu pia wanapaa kama Terminal 3 pale Julius Nyerere

Lakini bado adha ya joto kali la Jiji la Dar Es Salaam na baadhi ya foleni kwenye baadhi ya barabara inanipa takafuri jioni ya leo, bado fikra zangu ni Morrison namtazama vyema sana na ananikumbusha taswira nyingi sana

Ningependa kumpa stori za Adrian Mutu aliekubali kuogelea pesa za tajiri wa Chelsea pale London, ila nidhamu ndogo na fujo za nje ya uwanja alimaliza soka lake ingali tunamuhitaji sana, lakini si ni life bwana.

Kipaji kama cha Bernard Morrison kiliwahi kuwepo unamkumbuka Mario Balloteli? Wote wanaishi kwenye script moja iliyochorwa na Lamata, wote wanaishi njia moja kama watalaamu wa IT wanavyocopy na kupaste.

Kuna muda adha zetu ukisema kuhusu Morrison watu wanaweza kuona una nongwa tu, wakinuna sana watasema huna malezi ya pande mbili au ulitokeza miguu badala ya kichwa, labda foleni za Dar Es Salaam zinantia ukichaa Mimi

Adha za Dar Es Salaam zinanikumbusha namna alivyowavuruga Afrika Kusini, kuanzia utovu wa nidhamu alipogoma mpaka kwenda timu moja kwa mkopo licha ya kupokea malipo, lakini watu waliziba pamba na kusahau yote haya.

Juzi juzi nilisikia Simba imebadilika sana hakuna sajili za mizuka, lakini kwa unafki wangu labda mtasema, hivi Simba kilichobadilika ni nini?? Ni watu au ni mfumo?? Kwa upumbavu wangu labda niseme chupa mpya ila mvinyo ule ule, hakupaswa kuwa pale

Nilimsikia akipaita pale Chuo cha Soka, niliwasikia wakisema pale atabadili tabia yake, lakini mbona waneni walisema “Mtoto wa mbuzi kamba mali yake” wakamaliza na kusema “Asidi haachi asili” tuwe tunawasikiliza Wahenga, huwa wana maana muda mwingine.

Mnisamehe tu kama nimewakwaza ni adha tu za Dar Es Salaam zimeniwazisha haya! Nikifika Nyumbani wacha niwashe ITV yangu kisha niweke TBC yangu, nikifika nitatumia mlango kufungua funguo yangu, Adha zinachosha tu!


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

14 Komentara

    Atavuna alichopanda

    Jibu

    Maneno hayo tuu

    Jibu

    saf

    Jibu

    Morison yupo vizuri

    Jibu

    Morison mchezaji mzuli

    Jibu

    Morrison kama kawaida yake anawakeraaa tatizo ameshaona Simba wanamchukulia mchezaji wa kawaida hapati muda mwingi wa kucheza lazima atawazingua.

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Morrison hana inshu huyo

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Jamaaa anajua

    Jibu

    Morrison ni shida sana

    Jibu

    Huna jipya morrson kwisha habar yako

    Jibu

    Jamaa kama anavuta bangi

    Jibu

    Ni kweli mwandishi umenena

    Jibu

Acha ujumbe