Bernardo Silva Kuondoka Manchester City Mwisho wa Msimu

Kiungo mahiri Bernardo Silva anaripotiwa kuchukua uamuzi wa mwisho wa kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu huu, akifunga ukurasa wa safari yake ya mafanikio ya karibu miaka tisa ndani ya klabu hiyo. Nyota huyo wa Ureno ameeleza dhamira yake kwa uongozi wa klabu, akitafuta changamoto mpya baada ya mkataba wake kukaribia kumalizika.

Bernardo Silva Kuondoka Manchester City Mwisho wa Msimu

Katika kipindi chake Etihad, Bernardo ameandika historia kwa kushinda mataji sita ya Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa, akiwa sehemu muhimu ya mafanikio makubwa chini ya Pep Guardiola. Kuondoka kwake kutakuwa pigo kubwa kwa kikosi, si tu kwa uwezo wake uwanjani bali pia kwa uongozi wake ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.

Manchester City sasa wanajiandaa kwa maisha bila Bernardo, huku pia kukiwa na tetesi za Rodri kuhusishwa na Real Madrid. Ili kujaza pengo hilo, majina kama Sandro Tonali na Elliot Anderson yanatajwa kama mbadala wanaoweza kuleta nguvu mpya katikati ya uwanja.

Bernardo Silva Kuondoka Manchester City Mwisho wa Msimu

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa muda mrefu, Bernardo amekuwa akihusishwa na kuhamia Hispania, hasa FC Barcelona, ambapo ndiko anapopendelea zaidi. Hata hivyo, changamoto za kifedha za Barca zinaweza kuwa kikwazo, licha ya taarifa kuwa mchezaji yuko tayari kupunguza mshahara wake ili kufanikisha uhamisho huo.

Bernardo Silva Kuondoka Manchester City Mwisho wa Msimu

Mbali na Ulaya, vilabu vya Saudi Arabia na Marekani pia vinaonesha nia kubwa ya kumsajili kwa kumpa ofa nono. Wakati huo huo, City wanakabiliwa na presha ya kumaliza msimu kwa mafanikio, wakiwa nyuma ya Arsenal kwenye mbio za ubingwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.