Berrada Matumaini Kibao kwa Ten Hag

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Manchester United Omar Berrada amezungumza juu ya mipango ya klabu hiyo kuhakikisha wanairejesha kwenye kilele cha ubora wake wambao ilikua nao kwa miaka mingi iliyopita.

Omar Berrada amesema katika hilo msimu huu wamehakikisha wanaongeza ubora kwenye timu ya wanaume ambapo wameongeza wachezaji watano na kumpa ushirikiano wa karibu kocha wao Erik Ten Hag

“Tunataka kuirejesha klabu kwenye kilele cha soka la Ulaya.”

“Tumeimarisha timu yetu ya kwanza ya wanaume kwa wachezaji watano wenye msisimko na kuweka muundo mpya wa uongozi wa soka ili kutoa msaada mkubwa kwa meneja wetu, Erik ten Hag.”berradaMkurugenzi huyo aliendelea kuzungumza kwa kusema

“Sisi sote tumeelekeza nguvu kwa umoja katika kufanikisha mustakabali mzuri, huku mafanikio ya soka yakiwa kitovu cha juhudi zetu.”

“Lengo letu wazi ni kuirejesha klabu kwenye kilele cha soka la Ulaya ili kufanikisha mafanikio endelevu ndani na nje ya uwanja.”

Klabu ya Manchester chini ya Uongozi wa Omar Berrada kama mkurugenzi mkuu mtendaji wa klabu hiyo umeonesha nia ya dhati ya kuhakikisha wanapambana kuirejesha Manchester United kwenye ubora wake, Huku akisisitiza bado wana imani na kocha Erik Ten Hag ambaye ameonekana kutokuaminiwa na mashabikiwa klabu hiyo kwa kiwango kikubwa.

Acha ujumbe