Leslie Feinberg alikuWa mwandishi mkubwa sana nchini Marekani, licha ya kuwa na maumbile ya kike lakini alipenda sana kuwa mwanaume, hivyo ikambidi aishi katika desturi za kiume (Tom boy). Binti huyu aliandika article nyingi sana ikiwemo ya kuhusu Gender iliyoitwa -Transgender Liberation humu ndani kuna madini mengi sana kuhusu jinsia.

Aliwahi pia kunena kuwa “Gender is the poetry each of us makes out of the language we are taught.” Akimaanisha kuwa jinsia ni kama shairi, kila mtu analitunga kwa lugha aliyofundishwa. Shirikisho la soka la Ujerumani GFA liliishi katika misingi ya mwandishi huyu kwa kuwapa nafasi wanawake wengi katika michezo.

Bundesliga, Bibiana Mwanamke wa Kwanza Kuchezesha Bundesliga, Meridianbet
Bibiana Steinhaus katika mechi yake ywa kwanza Bundesliga

Nyota ikamuwakia binti Bibiana Steinhaus aliyependa kazi ya uaskari na uamuzi wa sheria 17 za soka, kumbuka huyu ni mpenzi wa referee maarufu duniani Howard Webb, Bibiana alipendwa na wengi tangu alipopata nafasi ya kuchezesha soka nchini Ujerumani.

Bundesliga, Bibiana Mwanamke wa Kwanza Kuchezesha Bundesliga, Meridianbet
Bibiana Akiwa na Webb

Jumapili ya tarehe 10 Septemba 2017 akaingia kwenye vitabu vya Bundesliga kama refa wa kike wa kwanza kuchezesha mechi ya Hertha BSC dhidi ya Wender Bremen, alipomaliza kuchezesha mechi hiyo, Bibiana alilia sana, kwani aliamini ile ndoto aliyoiota kila siku, imetimia. Bibiana alistaafu mara baada ya kuchezesha mechi kubwa.

Bundesliga, Bibiana Mwanamke wa Kwanza Kuchezesha Bundesliga, Meridianbet

Ni mechi ya Bayern Munichen dhidi ya Borusia Dotmund, ya September 30 mwaka 2020, ambapo Bayern alishinda kwa goli 3 – 2. Akiwa na umri wa miaka 41.Bibiana aliamua kustaafu kwakua tayari alishaweka alama kwenye mhuri wa Bundesliga, aliwahi kusema “Nawaachia vijana nao wapate ulaji”.

Bundesliga, Bibiana Mwanamke wa Kwanza Kuchezesha Bundesliga, Meridianbet

Bibiana ni miongoni mwa waamuzi wasafi kabisa, hakuwahi kukutwa na kashfa yoyote ya upangaji wa matokeo, alipoulizwa kuhusu nyakati ambayo hatoisahau, alijibu ile moment ambayo Taifa la Iran lilipopiga marufuku kuoneshwa kwa mechi zote atakazochezesha yeye.
Hii ni kwasababu Taifa hilo ni la kidini na haliruhusu wanawake kuonekana akiwa amevalia mavazi mafupi.

Hapa Tanzania namfananisha Bibiana na Bi Rukia, naye ni mwamuzi mzuri, asanteni Tff kwa kuishi kwenye misingi mizuri ya jinsia, wapo mabinti wengine mitaani wenye uwezo kama Bibiana, mkiwaangalia na wao, basi watalisaidia soka letu.


USHINDI UPI NI MKUBWA KWAKO, £2,000,000? 🤑

Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.

Bundesliga, Bibiana Mwanamke wa Kwanza Kuchezesha Bundesliga, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa