Bifu la Cantona na Deschamps na Kazi ya Mkude Isiyo na Thamani

Bifu kubwa zaidi duniani ni Viungo wa chini na wajuu hilo ni bifu la asili, ni bifu hili linawafanya Viungo wa chini kuonekana Punda na hakuna wanachofanya, weka nukta hapo

Eric Cantona ana bifu lake kubwa sana na Didier Deschamps, Wafaransa wawili hawa wasiopenda kabisa ni mwanzo waandishi walidhani labda ni battle of brilliance lakini ilikuwa ni battle of attitude.

Eric Cantona alikuwa na kitabia chake cha dharau kwa viungo wakabaji, sasa Deschamps anakaba mpira anawapa wao ila wanapoteza kirahisi sana, Deschamps akamwambia kwa Kifaransa “Pourquoi perdez-vous le ballon facilement”

Kwanini Eric unapoteza mpira kirahisi?? Ndicho aliuliza, Cantona alimwambia tu kazi yako wewe ni kukaba huko na kutupa sisi mpira Mafundi tuuchezee, ndicho hiki kilileta bifu kubwa sana, ni laana hii ikabaki kwa viungo wote wa chini.

Unamfahamu Jonas Mkude wa Simba?? Mnawaimba sana wakina Chama, ni dhambi hiyo, Mnawaimba sana wakina Miquissone ni dhambi hiyo, hamumtaji Mkude sana, tena tunaenda mbali na kusema ni Kiungo wa kazi moja tu, weka nukta hapo.

Mchezo kati ya Tanzania na Tunisia pale Taifa, kulikuwa na battle ya Jonas Mkude na Ferjani Sassi, Kiungo wa Zamalek na Tunisia huyo, gameplan za timu zote mbili kuna muda ziliategemea hawa, mwishowe sifa akazibeba Fei Toto na Wahbi Khazri.

Katika mchezo ule Ferjani wa Tunisia alipiga pass 63 za usahihi na tija sawa na 92% wakati huo Jonas Mkude alimfuatia na pass 62 sawa na 90% bahati mbaya hakuna aliewaona na hakuna aliewaimba watu hawa.

Mkude na Ferjani haikuwa tu mchezo bali Tactical battle and battle of brilliance, dunia inawasahau sana hawa.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

24 Komentara

    Asante kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Maisha yenyewe mafupi bifu la nini watu tufanyeni kazi tuache ujinga

    Jibu

    Duh! Ndo maisha yetu haya

    Jibu

    Bifu sio zuri jamn hasa iyo sekta ya michezo kwan wakiendeleza mabifu hawatakua na matokeo mazuri

    Jibu

    Maisha ya bifu si mazuri kabsaa

    Jibu

    Ni kawaida kwenye soka la Mpira au mahali popote penye watu wengi lazima vitu kama hivyo kutokea

    Jibu

    Hivi ni vitu vya kawaida kwenye watu wengi

    Jibu

    ni kitu cha kawaida kwny soka

    Jibu

    Haya maisha sio poa yanini kugombana

    Jibu

    Mabifu hayafai fanyeni kazi

    Jibu

    Asant kwa taarifa

    Jibu

    Mabifu sio kitu kizur

    Jibu

    Mabifu hayafai jamani.

    Jibu

    Bifu lao la muda sana

    Jibu

    Mabifu sio kitu mabifu uludisha nyuma vitu kwakweli

    Jibu

    Bifu sio nzuri sana.ishini kwa amani.

    Jibu

    Binadamu siku zote tunamusifia muhudumu aliyeleta chakula kitamu mezani, hatumbuki mpishi na mnunuzi wa vyakula

    Jibu

    Bifu sio zuri

    Jibu

    Nice information

    Jibu

    Si poa

    Jibu

    viongozi wao wanabidi wakae chini wasuluishe tofauti zao maisha na bifu si mazuri

    Jibu

    Kwann lakini

    Jibu

    Vizur

    Jibu

    Haya mambo kawaida sana

    Jibu

Acha ujumbe