Bingwa Rudisha Nje kwa Wiki 16!

Mshindi mara mbili wa michuano ya Olympic na ambaye anashikilia rekodi ya kushinda kukimbia mbio za umbali wa 800m duniani, David Rudisha atakaa nje ya uwanja kwa muda wa majuma 16! Hii imetokana na yeye kuumia kifundo chake cha mguu wa kushoto.

Mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 31 aliumia sehemu hiyo ya mwili wake akiwa kijijini kwao Kilgoris, magharibi mwa taifa la Kenya siku ya tarehe 19 mwezi Mei ambapo madaktari wake wanasema kuwa uchungizi wa karibu zaidi uligundua kuwa amepasuka kifundo cha mguu.

“Hatukuweza kufanya upasuaji kumtibu ambapo sasa mchezaji huyo atakuwa chini ya uangalizi maalum kwa siku moja inayofuata,” aliyasema hayo Victor Bargoria, ambaye ni mtaalam wa upasuaji, akiwaambia AFP, akaongezea kuwa itamchukua muda wa wiki 16 kwa mchezaji huyo kuanza tena mazoezi yake.

Rudisha, ambaye ameshinda rekodi ya 2012 London Olympics kwa muda wa saa 1:40.91, alikuwa anatarajiwa kurudi tena uwanjani baada ya kuwa ameumia goti ambapo ilimzuia kabisa kuchuana katika mashindano ya ubingwa wa dunia huko Doha mwezi Septemba.

Rudisha alikosa kushiriki michezoni kati ya mwaka 2013 pamoja na mwaka 2014 ikiwa ni matokeo ya kuumia mguu wake. Tunamtakia heri apone haraka!

39 Komentara

  Rudisha bonge la mwanariadha#meridianbettz

  Jibu

  Jamaa anatisha sanaa Yani hatari

  Jibu

  Kushikilia hiyo record mfululizo sio kitu kidogooo…tumuombee apone haraka

  Jibu

  Jamaa yuko vizuri san

  Jibu

  Pole sana mungu akupe afya upya urudi kambini

  Jibu

  Tunamtakia heri apone haraka

  Jibu

  Pole yake tunaomba apone haraka

  Jibu

  Pole bingwa Rudisha ,mungu akusaidie upone urudi kutumikia taifa.

  Jibu

  Apone aje andelee kutumikia taifa

  Jibu

  Pole sana atarud kama zamani

  Jibu

  Rudisha noma sana kweny liadha

  Jibu

  Pole sana..!bonge la mwanaliadha utarudi kama zamani

  Jibu

  mungu akupe afya urudi kambini

  Jibu

  Jamaha yupo vizuri huyo kwenye rihaza

  Jibu

  Pole sana kinaja, tunakutakia upone haraka

  Jibu

  Mwanariadha mahili

  Jibu

  so sad kwa rudisha

  Jibu

  Pole sana wiki kumi na sita sio nyingi sana atarudi tuu

  Jibu

  Yupo vizuri Sana mungu amjalie arudi dimbani

  Jibu

  Pole sana kwake

  Jibu

  Pole sn kjana

  Jibu

  Pole yake

  Jibu

  Pole Sana kwake atakaa sawa soon

  Jibu

  Mwanaliaza mzuri sana

  Jibu

  Mwenyez amsaidie

  Jibu

  Mungu amsaidie atapona

  Jibu

  Jamani pole yake#Meridianbettz

  Jibu

  Rudisha habari nyngne

  Jibu

  Pole yake jamani

  Jibu

  Rudisha yuko vizur sana

  Jibu

  get well soon

  Jibu

  Rudisha bonge la mwanariadha#meridianbettz

  Jibu

  Mungu amponye#meridianbettz

  Jibu

  Duh mungu atamsaidia

  Jibu

  Pole sana mungu atakusaidia#meridianbettz

  Jibu

  Mungu atamponya na atarudi ulingon

  Jibu

  Get well soon 🙏🙏

  Jibu

  Rudisha yupo vzr kwny kukimbizah upepo kila la heri atapona kwa uwez wa mungu🙏🙏🙏🙏🏼

  Jibu

  Pole yake sana

  Jibu

Acha ujumbe