Bissaka Kuongezewa Mkataba Mpya Man United

Beki wa klabu ya Manchester United Aaron Wan Bissaka huenda akaongezewa mkataba mpya wa kuenndelea kusalia ndani ya viunga vya Old Trafford.

Beki Bissaka anatarajiwa kumaliza mkataba wake msimu ujao na taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza Man United wanajiandaa kumpa ofa ya mkataba mpya beki huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye asili ya Congo.BissakaMan United wameshamuongeza mkataba Diogo Dalot ambaye ndio mshindani wa namba wa beki huyo, Hivo kutokana na taarifa hizo ni wazi kua Man United wameridhika na mwendendo wa mabeki hao wawili wa kulia klabuni hapo.

Beki Aaron Wan Bissaka alitaka kutolewa kwa mkopo mwezi Januari katika dirisha dogo lakini mabadiliko yake ya kiuchezaji ndani ya klabu hiyo ndio yamemfanya kocha Ten Hag kufikiria kumuongezea mkataba.BissakaBeki huyo kwasasa anaonesha utofauti mkubwa sana tofauti na miezi sita nyuma ambapo wengi waliamini beki huyo atatemwa, Lakini mpaka sasa dalili zinaonesha atasalia klabuni hapo kama kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

Acha ujumbe