Nahodha wa wekundu wa msimbazi Simba John Bocco, amesema kuwa wana kikosi bora jambo ambalo linawafanya wawe na imani ya kupata matokeo mbele ya Kaizer Chiefs kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Mei 15.

Bocco alikuwa ni miongoni mwa wachezaji 24 ambao walikwea pipa Mei 11 kuelekea Afrika Kusini kwa kupita Kenya kwa shirika la ndege la Kenya Airways aliliambia Championi Jumatano wana imani ya kufanya vizuri.

bocco simba

Mei 15 katika uwanja wa South Africa wa FNB, timu ya wekundu wa msimbazi Simba inayonolewa na kocha mkuu Didier Gomes itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu kwenye robo fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho la Africa CAF huku mechi ya pili itachezwa nyumbani kwa Simba Uwanja wa Mkapa Tanzania.

bocco

Bocco alisema:”Tuna kikosi imara kwa sasa na kila mchezaji anapenda kuona timu inapata matokeo hivyo tunawafuata wapinzani wetu tukiamini kwamba tunakwenda kusaka ushindi, mashabiki watuombee.

“Malengo yetu kushinda ili tuweze kufikia malengo ambayo tulikuwa tumejiwekea tangu mwanzo wa msimu hilo linawezekana na tunajua kwamba wapinzani wetu wapo imara ila hatuna mashaka tunawaheshimu,” .

Kwa sasa kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa siku ya Jumamosi Mei 15, 2021.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

bocco, BOCCO: Tuna Kikosi Bora Kinachotupa Matokeo Kimataifa, Meridianbet

CHEZA HAPA 

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa