Brahim Diaz Asaini Mkataba na Milan

Ni suala la muda tu kabla ya tangazo rasmi kwani Brahim Diaz ameripotiwa tayari ameshasaini mkataba na klabu ya Milan.

Mshambuliaji wa Real Madrid anawasili San Siro kwa mkopo wa miaka miwili wenye thamani ya €3m na kipengele cha kumnunua kwa €22m mnamo Juni 2023.

Calciomercato.com inaripoti kuwa Los Blancos wana kifungu cha kumnunua katika dili hilo kwa thamani ya euro milioni 27, sababu Brahim Diaz anarudi Rossoneri kwa angalau miaka miwili.

Brahim Diaz Asaini Mkataba na Milan
Brahim Diaz

Mchezaji huyo wa miaka 21, ambaye alihamia Real Madrid kutoka Manchester City Januari 2019, alitumia msimu wa 2020-21 kwa mkopo na Diavolo, wakati Milan wakimaliza katika nafasi ya pili kwenye Serie A.

Brahim alicheza michezo 39 ya mashindano yote msimu wa 2020-21, akichangia mabao saba na asisti nne katika mchakato huo.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe