Brazil imeanza sura mpya kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) kuthibitisha namba za jezi za kikosi chake cha wachezaji 26 kitakachosafiri kwa ajili ya mechi zijazo za kirafiki.
Raphinha amepewa jezi namba 10, akirithi namba hiyo iliyotawala kwa miaka zaidi ya 10 mgongoni mwa Neymar. Hatua hiyo inaonyesha nafasi kubwa ambayo nyota huyo wa Barcelona ameanza kupewa kwenye kikosi cha Selecao.

Namba hiyo imewahi kuvaliwa na mastaa wakubwa kama Pele na Ronaldinho, hivyo kumpa Raphinha kunaweka wazi umuhimu wake katika mpango mpya wa Brazil. Mchezaji huyo mwenye miaka 29 anatarajiwa kuwa mhimili wa ubunifu katika safu ya mbele.
Wakati Raphinha akichukua namba 10, Endrick amepewa jezi namba 9 iliyokuwa ikivaliwa na Matheus Cunha, ambaye hakuitwa kwenye kikosi hiki cha mapumziko ya kimataifa.
Uamuzi huo unaonyesha pia namna Brazil inavyomwandaa Endrick kuwa mshambuliaji wao wa muda mrefu. Kinda huyo wa Real Madrid sasa anapewa jukumu kubwa zaidi katika kizazi kipya kinachoanza kujengwa baada ya kumalizika kwa kampeni ya Kombe la Dunia.

Mabadiliko hayo hayaishii hapo. Estevao amechukua namba 11, huku Vinicius Junior akiendelea na namba yake ya saba. Nyuma, Marquinhos na Gabriel Magalhaes wamebaki na namba nne na tatu mtawalia, wakati Hugo Souza amepewa namba moja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kikosi hicho kinachoongozwa na Carlo Ancelotti sasa kitaanza ziara yake kwa kuikabili Australia mjini Townsville Ijumaa, kabla ya kurudiana na Socceroos huko Brisbane siku nne baadaye.
Ziara hiyo itafungwa kwa mchezo dhidi ya India mjini Kolkata, mchezo ambao utawapa Ancelotti nafasi ya kujaribu mchanganyiko mpya wa wachezaji na mifumo kuelekea majukumu yajayo ya Brazil.

Kwa Raphinha na Endrick, hizi ni hatua muhimu katika safari ya kuongoza kizazi kipya cha Selecao, huku jezi namba 10 na 9 zikianza kupata sura mpya baada ya enzi iliyotawaliwa na Neymar na Matheus Cunha.


