United wamekumbana na pingamizi jingine katika juhudi zao za kumsajili Bryan Mbeumo baada ya ofa yao iliyoboreshwa ya hadi £62.5 milioni kukataliwa na Brentford. Ofa hiyo mpya ilikuwa na £55 milioni taslimu pamoja na £7.5 milioni kama nyongeza kulingana na mafanikio. Hii imekuja baada ya ofa ya awali ya £45 milioni pamoja na hadi £10 milioni ya nyongeza kukataliwa mapema mwezi huu.
Brentford wameshikilia msimamo wao, wakiripotiwa kutaka kiasi sawa au zaidi ya kile Wolves walichopokea kwa Matheus Cunha (£62.5 milioni taslimu) kabla ya kumwachia Mbeumo, ambaye bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mbeumo ana thamani kubwa sokoni baada ya msimu mzuri uliopita ambapo alifunga magoli 20 na kutoa asisti 9, akivunja rekodi yake binafsi ya msimu. Licha ya hatari ya kumpoteza bure mwakani, Brentford wako tayari kumweka hadi wapewe dau linaloridhisha.
Manchester United tayari wameongeza nguvu ya ushambuliaji kwa kumsajili Matheus Cunha, lakini wanatamani kuongeza chaguo lingine mbele. Hata hivyo, huenda wakalazimika kuongeza dau lao au kulipa taslimu yote ili kuwashawishi Brentford — la sivyo, wawe tayari kupoteza nafasi hiyo kwa vilabu vingine vinavyomnyatia mchezaji huyo wa Cameroon.