Brighton Kumchukua Mturuki wa Fenerbahce

Klabu ya Brighton kutoka nchini Uingereza ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili beki wa kimataifa wa Uturuki ambaye anakipiga klabu ya Fenerbahce Ferdi Kadioglu.

Brighton wamekua kwenye mazungumzo na beki huyo wa kushoto wa Fenerbahce kwa takribani wiki mbili ambapo wamshafikia makubaliano kwa upande wa mchezaji huyo, Kwani klabu hiyo imefanikiwa kukubaliana maslahi binafsi na mchezaji huyo kilichobaki ni makubaliano na klabu ya Fenerbahce.brightonKlabu ya Fenerbahce imetaarifiwa na mchezaji Ferdi Kadioglu kua anataka kutimka klabuni hapo na kujiunga na klabu hiyo kutoka nchini Uingereza, Hivo klabu hiyo kutoka nchini Uturuki inasubiri dau kwa klabu ya Brighton ili kuweza kumaliza dili hilo  kabla ya dirisha kufungwa.

Beki huyo wa kimataifa wa Uturuki alikua anaviziwa kwa karibu na klabu ya Manchester United lakini mpaka sasa inaonekana klabu ya Brighton ndio kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumchukua Ferdi Kadioglu, Kilichosalia kwasasa ni kupeleka dau ambalo klabu ya Fenerbahce itakubaliana nalo.

Acha ujumbe