Brighton Kumuachia Undav

Klabu ya Brighton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza inaelezwa kufikia makubaliano na klabu ya Stuttgart ya nchini Ujerumni kwajili ya kumuuza  mshambuliaji Deniz Undav.

Stuttgart wameonekana kuvutiwa na uwezo ambao Undav ameuonesha ndani ya klabu hiyo kwa kipindi alichodumu ndani ya timu hiyo kwa mkopo akitokea Brighton msimu uliomalizika 2023/24, Hivo ndio wanataka kuhakikisha wanapata huduma ya mchezaji huyo raia wa kimataifa wa Ujerumani.brightonStuttgart inaelezwa kutoa kiasi cha Euro milioni 30 kwajili ya mshambuliaji Deniz Undav huku ikielezwa vilabu hivyo viwili vimeshafikia muafaka, Hivo mpaka sasa ni suala la muda tu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kutangazwa kujiunga na klabu ya Stuttgart.

Mshambuliaji Undav ameonesha kila dalili ya kujiunga na klabu ya Stuttgart akitokea Brighton hii imearahisisha ushamisho huu kwa kiwango kikubwa, Kwani mchezaji mwenyewe ameonesha kua anataka kujiunga na klabu hiyo kutokana nchini Ujerumani.

Acha ujumbe