Brighton Yashusha Kifaa Kutoka Uholanzi

Klabu ya Brighton Hove and Albion iko mbioni kukamilisha dili kiungo wa klabu ya Feyernoord  Mats Weiffer raia wa kimataifa wa Uholanzi kwa ada ya uhamisho ya Euro €30 milioni.

Brighton wanahitahiji kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao baada ya kutokua na msimu mzuri wa mwaka 2023/24, Jambo ambalo limewafanya kuingia kwa hasira sokoni kwajili ya kukamilisha sajili zao mapema na msimu ujao warudi kwenye ubora.brightonMsimu uliopita klabu hiyo iliyokua chini ya kocha Roberto de Zerbi haikua na wakati mzuri sana kwenye ligi hiyo jambo ambalo lilifanya klabu hiyo kuachana na kocha huyo raia wa kimataifa wa Italia, Klabu hiyo lengo kubwa ni kurejesha makali yake msimu ujao.

Mats Weiffer amekua kwenye kiwango kizuri ndani ya klabu ya Feyernoord ya nchini Uholanzi kitu kilichowafanya mabosi wa klabu ya Brighton kuwinda saini yake na mpaka sasa wako kwenye hatua za mwisho katika kukamilisha dili hilo ambalo litagharimu ya €30miilioni.

Acha ujumbe