Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Armando Broja anatarjiwa kua nje kwa msimu mzima uliobakia baada ya kupata majeraha ya enka na kulazimika kufanyiwa upasuaji.

Mshambuliaji Broja ambaye alikua kwa mkopo katika klabu ya Southampton msimu uliomalizika huku akigeuka kua miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha mwalimu Graham Potter atakosekana kwa msimu mzima uliosalia.brojaKlabu ya Chelsea imekua ikikubwa na majeruhi mara kwa mara kwa siku za hivi karibuni kitu ambacho kimeifanya klabu hiyo kupitia wakati mgumu zaidi kwenye michezo yake kutokana na idadi kubwa ya majeraha kwenye kikosi chake.

Klabu ya Chelsea imepokea taarifa za Armando Broja kwa masikitiko kwani kwenye kikosi washambuliaji walikua wawili, Ambapo kwasasa amebakia Aubameyang ambaye anaoekana bado hajarudisha makali yake vizuri tangu ajiunge klabuni hapo.brojaKlabu ya Chelsea imepokea taarifa njema kwa siku za hivi karibuni baada ya beki wake waliomsajili kwenye dirisha liliopita kutoka Leicester Wesley Fofana kurejea rasmi kwenye kiwanja cha mazoezi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa