Bruno Fernandes Ampakulia Minyama Kinda Man United

Nahodha wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes amempakulia minyama kinda wa klabu hiyo Kobbe Mainoo ambaye amecheza vizuri katika mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Arsenal.

Bruno Fernandes baada ya mchezo wa jana amesema kinda Mainoo ni mchezaji mzuri sana na bado kijana mdogo hivo ana nafasi zaidi ya kuboresha kiwango chake kutokana na uwezo ambao anauonesha kwasasa.Bruno fernandesKinda Kobbe Mainoo amekua kwenye kiwango kizuri mpaka sasa ambapo katika michezo mitatu ya kujiandaa na msimu ambayo klabu ya Man United imecheza mpaka sasa mpaka kumfanya nahodha Bruno Fernandes kumsifu kutokana na uwezo wake.

Kobbe Mainoo ambaye ametoka kwenye akademi ya Manchester United ni kijana ambaye anatabiriwa kufanya makubwa siku za usoni kutokana na ubora ambao alianza kuonesha akiwa kwenye timu za vijana za klabu hiyo mpaka sasa kwenye timu ya wakubwa.Bruno fernandesKocha wa Manchester United Erik Ten Hag inaelezwa anavutiwa zaidi na kijana huyo mwenye kipaji kikubwa ambapo anaamini kijana huyo atafanya mambo makubwa mbeleni na mpango wake ni kumpa dakika zaidi za kucheza msimu ujao.

Acha ujumbe