Bruno Fernandes Kusaini Mkataba Mpya United

Nahodha na kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes inaarifiwa yuko mbioni kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo kabla ya dirisha hili kubwa kufungwa.

Bruno Fernandes inaelezwa ataongeza mkataba mpaka mwaka 2027 ambao kutakua na kipengele cha kuongeza mpaka mwaka 2028, Mkataba wa mchezaji huyo ulikua unamalizika mwaka 2026 hivo anaongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi ambao utakua na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine.bruno fernandesKiungo huyo wa kimataifa wa Ureno amekua kwenye kiwango bora kwa muda mrefu ndani ya Manchester United tangu ajiunge klabuni hapo mwaka 2020 mwezi Januari,  Ambapo mwaka 2022 aliongeza mkataba wa miaka minne ambao utamueka klabuni hapo mpaka 2026 a sasa wanataka kuufanyia maboresho na kuongezwa mpaka 2027.

Kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha Bruno Fernandes ndio sababu ya mabosi wa klabu ya Manchester United kutaka kumuongezea mkataba mwingine kabla ya ule wa awali kumalizika, Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno inaelezwa mkataba mpya atakaousaini utaweza kumfanya kua moja ya wachezaji wanaolipwa zaidi klabuni hapo.

Acha ujumbe