Bruno Guimaraes Bado Nipo Newcastle

Kiungo wa kimataifa wa Brazil ambaye anakipiga ndani ya klabu ya Newcastle Bruno Guimaraes ameweka wazi hana mpango wa kutimka ndani ya klabu hiyo licha ya tetesi zinazoendelea.

Bruno Guimaraes amekua akihusishwa na vilabu kadhaa ikiwemo klabu ya Manchester City, pamoja na klabu ya Arsenal lakini kiungoi huyo amekkanusha kua hana mpango wa kutimka ndani ya viunga vya St. James Park kwani ana furaha ya kuendelea kuwepo ndani ya timu hiyo.bruno guimaraes“Nina furaha sana kuwa Newcastle, sikuwahi kusema ningependa kuondoka!”

“Siku zote nimesema ningependa kuweka jina langu katika historia ya klabu. Siwezi kusubiri kufanya bora zaidi kwa ajili ya klabu na mashabiki.”

Kiungo Bruno Guimaraes amekua na kiwango bora sana ndani ya kikosi cha Newcastle tangu ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa, Jambo ambalo limemfanya kua kwenye orodha ya wachezaji ambao wanafukuziwa kwa karibu na vilabu kama Arsenal, pamoja Manchester City lakini msimamo wake uko wazi ni kuendelea kubaki ndani ya Newcastle United.

 

 

Acha ujumbe