UONGOZI wa Yanga kupitia Afisa habari wake Hassan Bumbuli umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kwenye mechi zao ambazo zimebaki ili kukamilisha ratiba kwa msimu wa 2020/21 na kupata kile ambacho wanakitarajia.

Yanga kupitia Bumbuli iliweka wazi kwamba inahitaji kutwaa taji la Kombe la Shirikisho pamoja na ligi. Na mataji yote hayo mawili mabingwa watetezi ni Simba.

Ikiwa itashinda mbele ya Biashara United kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho wa nusu fainali inaweza kukutana na Simba au Azam FC ambazo zitakutana nazo kwenye mchezo wa nusu fainali.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara imecheza jumla ya mechi 29 imebakiwa na mechi tano ambazo ni dhidi ya Ruvu Shooting, Juni 17, Mwadui FC, Juni 20, Simba, Julai 3, Ihefu Julai 14 na kigongo cha mwisho ni dhidi ya Dodoma Jiji, Julai 18.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa:”Michezo minne imebakia kwa sasa, ambapo ni ule wa tarehe 17, 20 pia Kombe la FA tarehe 24. Mingine ni dhidi ya Ihefu na Dodoma ila tutaiwekea mipango namna ya kurudi baada ya kumaliza kwenye chezo wa Kombe la Shirikisho,”.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa