Sir Stirling Moss alikuwa mmoja kati ya wanamichezo wakongwe wa mbio za magari. Alizaliwa Kensington mwaka 1929. Alikuwa mmoja wa madereva bora zaidi kuwahi kutokea kwenye michuano ya Formular 1 wa wakati wote. Wanamichezo wa tasnia hii na wengine wote wanaungana kumuaga akiwa amefariki katika umri wa miaka 90. Buriani Sir Stirling Moss.
Legendari huyu alistaafu mbio za magari mwaka 1961, na akastaafu kushiriki shughuli za umma rasmi mwaka 2018 kwa sababu ya shida ya afya. Aliiumwa kwa mda mrefu kabla ya umauti kumkuta. Anakumbukwa kwa mchango na ushiriki wake mkubwa katika Formular 1 hata kama hakuwahi kuchukua Ubingwa wa Dunia.
Alipata maambukizi ya kifua alipokuwa Singapore kwa ajili ya likizo Disemba 2016. Alitumia siku 134 za hivi karibuni katika matibabu hospitali.
Mwanatimu mwezie na Moss alibainisha kuwa, huyu ni legendari ambaye hajaacha alama kwenye mbio za magari, bali amechangia kwa kiasi kikubwa kuzaliwa kwa vipaji vipya kwanye tasnia hiyo, baadhi yao wamechukua ubingwa wa dunia.
Moss alishinda jumla ya mbio 16 kati ya mbio 66 za F1 alizoshiriki kati ya mwaka 1951 na 1961, na mwaka 1955 alikuwa muingereza wa kwanza kushinda Home Grand Prix akiwa Aintree. Amefariki Jumapili ya pasaka akiwa nyumbani kwake.
Rehema
Hii makala ni big up Safi sn meridianbet mnazid kunipa habari mzuri