Burnley Waomba Kuahirishwa kwa Mchezo wao Dhidi ya Watford

Klabu ya Burnley  wameiomba bodi ya ligi kuu Uingereza kuweza kuahirisha mchezo wao wa kesho Jumanne dhidi ya Watford kutokana na kuwa na visa vya maambukizi ya Uviko-19 na idadi ya majeruhi waliyonayo.

Bodi ya ligi inatarajiwa kukaa kikao baade leo siku ya Jumatatu ili kuweza kupitia maombi hayo ya klabu ya Burnley, ambayo yamekuja baada mchezo dhidi ya klabu ya Leicester kuahirishwa siku ya jumamosi.

Burnley

Waraka uliotolewa na klabu hiyo ulisomeka, “Burnley Football Club inathibitisha ya kupeleka maombi kwa bodi ya ligi ya kuomba kuahirishwa kwa mchezo wake wa siku ya jumanne usiku dhidi ya Watford nyumbani.”

Klabu ya Burnley mchezo wake wa jumamosi ulikuwa ni mchezo wa nne kuahirisha kutokana na sababu ya Uviko-19 ikiwa nchezo wa kesho ukiharishwa basi utakuwa mchezo watano, tokea waombe mara ya kwanza KUahirishwa kwa mchezo dhidi ya klabu ya Turf Moor.

Mchezo wa kesho awali ilibidi uchezwe tarehe 15 December lakini uliahirishwa na kupangiwa tarehe nyingine baada ya klabu ya Watford kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya Uviko-19.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe