Yohan Cabaye anasema kuwa anataka kuendelea kucheza soka hata mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake klabuni Saint-Etienne.
Mkataba wake unafikia ukomo ifikapo tarehe 30 Juni mwaka huu na anataka kuwa na Les Verts ama kwingine kokote.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 ni mshindi mara mbili akiwa na LOSC mwaka 2011 na bingwa wa Ligue 1 Conforama akiwa na klabu ya soka ya PSG mwaka 2014 na mwaka 2015, alicheza mara 12 kwa ajili ya klabu ya soka ya Saint-Etienne katika msimu ambao alikumbwa na majeraha na kisha ikafuatiwa na janga la Covid-19.
Cabaye aliwaambiwa L’Equipe: “Ninataka kuendelea kucheza soka na sitaki kabisa kusikia habari za kustaafu kwangu. Wakati huu ambao haturuhusiwi kucheza nimejipima na kuona kwamba hali yangu katika soka ikoje. Ninaikumbuka sana michezo yetu ya mpira wa miguu.
Imenifanyia mema mengi sana. Kutoka katika kujiwazia mimi mwenyewe hadi mpaka kufikia kucheza soka la kiushindani haswa, kuona soka la ushindani la wikiendi iliyopita huko Bundesliga, hata kama ikichezwa bila ya uwepo wa mashabiki basi ule utaratibu wa mwanzo wa asili utapotea kabisa. Ninataka kucheza soka. Iwe ni pale Saint-Etienne ama kwingine kokote kule. Mkataba wangu unafikia ukomo ikifika mwezi Juni 30 mwaka huu na hakuna ambalo limeamuliwa kati yetu mpaka sasa hivi.”
Klabu ya soka ya Saint-Etienne imepangwa kumenyana na klabu ya zamani ya Cabaye, PSG katika hatua ya fainali ya kuwania kombe la Coupe de France lakini haipo wazi endapo mchezaji huyo wa kimataifa wa taifa la Ufaransa ataendelea kuwa katika klabu yake wakati fainali ikifika.
Mchezaji Cabaye alisema: “Kocha Claude Puel aliongea nami kuhusu kuongeza mkataba wangu klabuni hapo na kisha akaongelea suala hilo mbele ya jamii yote. Tupo katika mazungumzo kwa sasa na sijafunga milango ya kusajiliwa tena ama kusaini mkataba mpya. Tutaangalia kitakachotokea kwetu. Kwa sasa sipingani na lolote lililo mbele yangu.”


Theckla
Bado ana uwezo mzuri na maamuzi yake yako sahihi
SADICK
Cabaye ni bonge la Kiungo#Meridianbettz
Gabriel
Jamaa mpira uko damuni cabaye yuko sahihi
Adelta
Cabaye Ni mchezaji mzuri sana
David pere
Anajikongoja tu kutafuta pesa lakini kusema kweli just limezama
mathayo sonje
Cabaye astaaf tu umri ushamtupa mkono maana majeruhi yamezidi bora apumzike
Theonestina
Jamaa anaujua mpira huyo
Lombo
duuh
aisha
Muacheni aendelee umri wake unaruhusu
Mwanaidi
Anakosea kwasababu ni jambo la busara sana kama muda wako wa kustaafu umefika hlf ukatae kwasababu kuna wengine wanaihitaji hiuo nafasi hivo kama muda wakustaafu umefika basi ni vyema angeachia ngazi tuu awapishe wengine
Mwanaidi
Anakosea kwasababu ni jambo la busara sana kama muda wako wa kustaafu umefika hlf ukatae kwasababu kuna wengine wanaihitaji hiyo nafasi hivo kama muda wakustaafu umefika basi ni vyema angeachia ngazi tuu awapishe wengine
Emmy cleopa
Cabaye ni mchezaji mnzur
Mariam mtandama
Duuuh
Povel
Yohan cabaye ni bonge la kiungo ni Jambo la busara kuendeleah kukipgah iliawez kuwap uzoefu na kujifunza kwa wanao chipukiah kupitiah kwake thnks meridian kwa gud news
Devotha
Kama anauwezo mzuri aendelee kucheza
Rehema Dickson
Sio sawa kama muda wa kustaafu umefika ni bora afanye ivyo itakua busara Sana
Zeiyana iddi
Mpira upo ndani ya damu..!ila unaweza kustaf theni uwe kocha kwenye timu ndogo ndogo ili wengine wajifunze kupitia wew..!
Evaluziga
Jamaa anajua Sana mpira
Hope mwaikuka
Anaweza
Antony Luseno
Kama umri unaruhusu aendelee
Shafii
Kuna maishaa baada ya mpira kama umri umekutupa mkono fanya mambo mengine
felister
waachie na wengine muda wako wa kustaafu umefika kampumzike
Swai
Kuna maisha mengine kama umri wake umeenda afanye kingine
Magdalena
Yupo vizuri Sana Ila umri ukisogea kustaafu ni lazima
Neema hassan
Umri umeenda aache tamaa..
Neema juma
Kama bado ana nguvuu aendelee tu
winfrida
cabaye yuko vizuri sana
Aziza mushi
Cabaye yupo sahihi
Hamidu
Kiungo fundi# meridianbettz
Ester mmakasa
Asante kwa taarifa meridianbet.
Ernest
Cabaye bado yupo vizuri sanaaa
Genia Sikaluzwe
Ahsant sana meridianbet kwa taarifa
mwakalosi
moja,ya kiungo bora wa chini lakini akikosea sana kwenda kucheza,ligi ya kwao
frank patrick
Akipige tu ila kuna muda mpira utamkataa kulingana na umri
Amani
Bado ana uwezo mzuri na maamuzi yake yako sahihi
Samiah
Umri unaruhusu mwacheni aende
Edgar
yupo vzr
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa