CAF : Mashabiki 35,000 Waruhusiwa Simba v Red Arrows.

 

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 35,000 kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Red Arrows utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

 

Uongozi wa klabu ya Simba SC umepokea barua rasmi kutoka CAF ikiwa na maelekezo hayo ambayo wanapaswa kuyafuata.

CAF imekuwa na utaratibu wa kuruhusu idadi fulani ya mashabiki kuingia uwanjani kwa ajili ya kujikinga na janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

Pamoja na mambo mengine, CAF imesisitiza kufuatwa kwa taratibu zote za kujikinga na ugonjwa huo kama kukaa kwa nafasi baina ya mtu na mtu na kuvaa barakoa kwa kila atakayehudhuria.

Tayari viingilio vya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Red Arrows vimewekwa wazi ambapo Mzunguko Sh 5,000, VIP B na C Sh 20,000 na VIP A Sh 40,000.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe