Gwiji wa Brazil Cafu amemsifu nyota wa Liverpool Trent Alexander-Arnold kama mmoja wa mabeki bora zaidi wa kulia duniani. Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akifanya vyema tangu alipoanza kucheza kikosi cha kwanza.

Alexander-Arnold amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Reds ambacho bado kinawania kutwaa mataji matatu na Cafu ameshangazwa na maendeleo yake.

 

CAFU, Cafu : Alexander-Arnold Beki Bora wa Kulia., Meridianbet

Cafu aliiambia BBC Sport: “Nimekuwa nikimfuatilia Alexander-Arnold misimu kadhaa akiwa Liverpool. Maendeleo yake katika miaka michache iliyopita yamekuwa ya kushangaza na kwa hakika ni mmoja wa mabeki bora zaidi wa kulia duniani.

“Ni mdogo, ana nguvu na amekua kwa kiasi kikubwa ukizingatia umri wake. Pia ana uzoefu mkubwa na ninaona mengi yanayofanana kati yake na mimi.

“Wote tunafanana kujitolea kushambulia, kwenda mbele na kuwa na ujasiri wa kupiga na kuweka krosi. Nyendo za mshazari anazofanya uwanjani pia zinafanana na nilivyokuwa nikifanya kama mchezaji.” aliongeza.

Alexander-Arnold, 23, amecheza mechi 45 katika mashindano yote msimu huu, akitoa mabao mawili na asisti 19 kwa Liverpool, tayari amebeba Kombe la Carabao na Kombe la FA chini ya Jurgen Klopp msimu huu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa