Kiungo wa klabu ya Chelsea Moises Caicedo imeelezwa amepata majeraha ya goti na hataweza kupatikana katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Bournamouth.
Kocha Mauricio Pochettino wakati anaongea na wanahabari amesema kua kiungo huyo amepata majeraha ya goti, Hivo wanahitaji kufanya uchunguzi zaidi siku za mbele lakini hatakuepo kwenye mchezo wa leo.Kiungo Moises Caicedo bado hajawa na mwanzo mzuri ndani ya klabu ya Chelsea na anapata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa siku ambazo hazijawekwa wazi mpaka sasa.
Kiungo huyo raia wa kimataifa wa Ecuador anatarajiwa afanye makubwa ndani ya klabu hiyo kutokana na gharama kubwa ambayo amesajiliwa nayo kutoka klabu ya Brighton and Hove Albion mwishoni mwa dirisha kubwa lililopita.Taarifa rasmi ya madaktari wa klabu a Chelsea inatarajiwa kutokana ili kueleza ni muda gani ambao kiungo huyo atakosekana uwnajani, Lakini kwa namna ambavyo kocha Pochettino ameeleza inaonekaana sio jeraha kubwa ambalo litamueka Caicedo nje ya uwanja kwa muda mrefu.