Calafiori ni Mali ya Arsenal

Beki wa kimataifa wa Italia ambaye anakipiga klabu ya Bologna Riccardo Calafiori inaelezwa ameshakubaliana kila kitu na klabu ya Arsenal kilichobakia ni kujiunga na washika mitutu hao wa London.

Calafiori alikua akigombaniwa na vilabu vitatu ambavyo ni Arsenal, Chelsea, pamoja na miamba ya soka nchini Italia klabu ya Juventus lakini mpaka sasa washika mitutu wa London ndio wanaonekana kushinda vita hii ya kumpata beki huyo mwenye uwezo mkubwa.CalafioriBeki huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka (22) amekua na msimu bora sana ndani ya ligi kuu ya Italia akiitumikia klabu ya Bologna ambapo alikua mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha kocha Thiago Motta mpaka wanafanikiwa kufuzu ligi ya mabingwa barani ulaya.

Klabu ya Arsenal imekubali kutoa kiasi cha €50 milioni ambayo ndio thamani ya beki huyo mwenye kipaji kikubwa kutoka nchini Italia, Hivo klabu ya Bologna ndio inasubiriwa kwasasa kuidhinisha mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo katika dirisha hili kubwa.CalafioriBeki Calafiori atakua na msaada mkubwa sana ndani ya kikosi cha Arsenal ambapo ataongeza ubora katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo, Kwani beki huyo ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani akicheza kama beki wa katikati lakini pia ana uwezo wa kucheza kama beki wa pembeni kushoto.

Acha ujumbe