Windo la Real Madrid, Eduardo Camavinga ametoa taarifa mpya juu ya hatma yake na uwezekano wa kuondoka Rennes.

Nyota huyu mwewnye uraia wa Ufaransa, anajiandaa kuungana na kikosi cha Didier Deschamps kwa ajili ya Michuano ya Ulaya mwezi ujao, huku taarifa juu ya uhamisho wake na wapi atakuwepo msimu ujao zikishika kasi.

Licha ya staa huyu, kinda wa miaka 18 kuhusishwa na kuhamia mji mkuu wa Hispania kwa dau linalotajwa kuwa €65m, Camavinga anadai kuwa yeye kwa upande wake bado hajafikia hatua ya kufanya maamuzi kamili.

“Inafanya ujisikie vizuri sana kujua timu kama Real Madrid au Bayern zinavutiwa na hali yako. Sitaweza kudanganya, bado sijaamua na familia yangu nini ambacho nitafanya.”

Real Madrid wanalitajwa kuwa walipewa dau la €75m kumnasa Vamavinga msimu uliopita, lakini dau lake kwa sasa linaonekana kubadilika baada ya mazungumzo ya mkataba na Roahzon Park mwaka 2020.

Wakati Real Madrid wakitarajiwa kufanya usajili mkubwa kuboresha kikosi cha Zidane, Camavinga anatarajiwa kuungana na David Alaba kuwasili klabuni hapo.


Pesa Ipo Hapa Katika Kasino ya Lucky Lucky.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Camavinga, Camavinga: Bado Sijafanya Maamuzi ya Hatma Yangu, Meridianbet

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa