Camavinga Kufanyiwa Vipimo Leo

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Eduardo Camavinga anatarajia kufanyiwa vipimo leo kutokana na majeraha ya msuli aliyoyapata katika mchezo wa jana dhidi ya Liverpool.

Camavinga hakufanikiwa kumaliza mchezo jana dhidi ya Liverpool kwenye ligi ya mabingwa ulaya ambapo waliambulia kichapo cha mabao mawili kwa bila dhidi ya Liverpool, Hivo kiungo huyo anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa klabu hiyo kuangalia majeraha hayo yatakua ni ya muda gani ili waweze kutoa taarifa kwa benchi la ufundi na mashabiki wa klabu hiyo.

camavinga

Kiungo huyo alipata majeraha ya goti mwanzoni mwa msimu huu na kumfanya kukosa michezo kadhaa lakini alifanikiwa kurejea uwanjani na kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa kiwango bora, Lakini kupata kwake majeraha tena jana imezua hofu kwa klabu hiyo kwani idadi ya majeraha klabuni hapo imekua sio ya kawaida.

Real Madrid wanapitia kipindi kigumu kwelikweli kutokana na majeraha ambayo yanaiandama timu hiyo kuanzia safu yao ya ulinzi, kiungo, na eneo la ushambuliaji, Hivo kama itabainika Camavinga na yeye amepata majeraha ya kumuweka nje ya uwanja itakua ni pigo lingine kwa kwa mabingwa hao wa ulaya.

Acha ujumbe