Cancelo Aitolea Uvivu Man City

Beki wa klabu ya Man City anayekipiga klabu kwa mkopo klabu ya Barcelona Joao Cancelo ameitolea uvivu klabu yake ya City kutokana na tuhuma ambazo amekua akitupiwa.

Cancelo ambaye anakipiga ndani ya Barcelona kwasasa amekua akizungumziwa tofauti ndani ya klabu ya Manchester City kwa namna ambavyo ameeleza beki huyo, Hii ikiwa ndio sababu ya beki huyo kuweka mambo hadharani.canceloBeki huyo ameeleza kua “Sikua mchezaji mwenye nidhamu mbaya ndani ya City kama ambavyo taarifa za uongo zinaeleza, Kuna wakati nilivamiwa nyumbani lakini kesho yake nilienda kuitumikia City dhidi ya Arsenal Emirates kuna vitu ambavyo huwezi kusahau kwani nilimuacha binti yangu na mke wangu wakiwa bado wana hofu lakini nikaenda¬† kuitumikia City”

“Manchester City watakua sio wenye shukrani kama wanaweza kunizungumzia kwa namna mbaya hivi, Kwani nimekua mchezaji muhimu kwao” Hii ndio kauli ambayo ameitoa beki huyo akionesha kutoridhishwa na taarifa zinatoka kumhusu ndani ya City.canceloBeki Joao Cancelo licha ya kua ni mali ya klabu ya Manchester City bado lakini kwa namna ambavyo amekua anaelezea maisha yake ndani ya City, Inaonesha wazi kua hana mpango wa kurudi ndani ya timu hiyo lakini vilevile ameshaweka wazi mpango wake ni kuendelea kuitumikia ndani ya klabu ya Barcelona.

Acha ujumbe