Beki wa kimataifa wa Ureno, João Cancelo, ameibua mjadala mkubwa kuhusu mustakabali wake baada ya kuonyesha wazi kuwa yupo tayari kupunguza mshahara ili kurejea kwenye klabu yake ya utotoni, Benfica. Kauli hiyo imekuja katika sakata lake la usajili huku akiwa kwa mkopo FC Barcelona akitokea Al-Hilal.

Cancelo, mwenye umri wa miaka 31, anaendelea kuonyesha kiwango kizuri Hispania akiwa amechangia bao moja na asisti nne ndani ya mechi 12 tangu alipojiunga mwezi Januari. Barcelona wanapenda kumbakisha moja kwa moja, lakini mkataba wake na Al-Hilal hadi 2027 unafanya mazungumzo kuwa magumu zaidi.
Akizungumza kwa hisia kubwa, Cancelo alikiri kuwa kurejea Benfica si suala la pesa bali ni mapenzi ya dhati. Amesema tayari amepata fedha nyingi kuliko alivyotarajia, na kwamba kucheza Benfica ni kwa ajili ya moyo wake, jambo linalomfanya awe tayari kukubali mshahara mdogo ili tu atimize ndoto hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, uhamisho wa kudumu kuelekea Barcelona bado una vikwazo, kwani Al-Hilal wanataka kurejesha fedha waliomnunulia kutoka Manchester City. Hii inawaweka Barcelona kwenye wakati mgumu kutokana na hali yao ya kifedha, huku Benfica nao wakipewa nafasi ya kuingilia dili hilo kufuatia kauli ya mchezaji.

Wakati huu, Cancelo anapaswa kuweka kipaumbele kwenye majukumu yake ya sasa, huku Barcelona wakiongoza La Liga na kujiandaa na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid. Mwisho wa msimu huu utaamua mwelekeo wake, kati ya kubaki Barcelona, kurejea Benfica, au kuanza safari mpya kabisa.



