Carlo Anchelotti: Ushindani ni Mkubwa Ndani ya Real.

Kocha wa klabu ya Real Madrid na mabingwa watetezi wa ulayab Carlo Anchelotti amesema klabu hiyo ima ushindani mkubwa kocha huyo amezungumza kauli hiyo baada ya kuulizwa kuhusu mchezaji wake Eden Hazard.

carlo anchelottiCarlo Anchelotti kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya kombe la ulaya amefunguka na kusema “Anajua hali ilivyo vizuri, Kila mchezaji anajua hali ilivyo hapa kuna ushindani mkubwa”Carlo Anchelotti akimzungumzia Hazard

Mchezaji Eden Hazard amekumbana na kipindi kigumu tangu ajiunge klabuni hapo majira ya joto mwaka 2018 kutoka klabu ya Chelsea akikosa nafasi ya kudumu kwenye timu hiyo, Hii inatokana pia na kuandamwa sana na majeruhi kwa Eden tangu ajiunge klabuni hapo.

carlo anchelottiEden Hazard mpaka sasa msimu huu amecheza dakika 158 katika klabu hiyo huku akiwa ameanza michezo isiyozidi miwili kwenye timu hiyo. Huku akikabiliwa na ushindani mkubwa kwenye nafasi anayocheza mpaka kocha huyo akaamua kumtumia kama chaguo la pili la Karim Benzema baada ya ushindani kua mkubwa katika eneo la pembeni.

Acha ujumbe