Rais wa mpito wa Barcelona – Carlos Tusquets ameibuka  na kuzungumzia suala la Lionel Messi. Kwa upande wake, angemuuza Messi katika dirisha la usajili lililopita.

Mapema mwezi Agosti, Lionel Messi aliomba kuondoka Barcelona kwa sababu mbalimbali. Licha ya kuwa habari hii iliuteka ulimwengu wa soka na kuzua taharuki miongoni mwa mashabiki na wadau wa Barca, Messi alijikuta akilazimika kubaki Barcelona.

Carlos Tusquets anasababu zake ambazo anadhani kutokana na sababu hizo, ulikuwa ni wakati sahihi wa kumuuza Messi.

Carlos Tusquets, Carlos Tusquets “Ningemuuza Messi Usajili Uliopita”, Meridianbet
Raisi wa mpito wa Barcelona – Carlos Tusquets.

Akizungumza na kituo cha redio cha RAC1, Tusquets amenukuliwa akisema “Kwa sababu za kiuchumi, ningemuuza Messi majira ya kiangazi.

“Hii ingeokoa sehemu kubwa ya mishahara na ingeongeza mapato kwa kiasi kikubwa. Lakini hili ni suala ambalo makocha wanatakiwa kuliridhia, hiyo sio sehemu yangu.

“Kwa sasa, LaLiga ndio wanaopanga viwango vya mishahara, ila kwa sababu hiyo ingesaidia.”

Carlos Tusquets, Carlos Tusquets “Ningemuuza Messi Usajili Uliopita”, Meridianbet
Lionel Messi

Manchester City ni kati ya timu zilizotajawa kuiwania saini ya Messi bila mafanikio na kwa siku za karibuni, usajili wa Messi kutua kwenye EPL umekanushwa vikali na Man City kwa sababu za kiuchumi na umri wa Messi.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Carlos Tusquets, Carlos Tusquets “Ningemuuza Messi Usajili Uliopita”, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

21 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa