Carrasco Awindwa Saudia Arabia

Winga wa klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania raia wa kimataifa wa Ubelgiji Yannick Carrasco anawindwa kwa karibu na klabu ya Al Shabab inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia.

Klabu ya Atletico Madrid inaelezwa inasubiri ofa rasmi kutoka klabu ya Al Shabab ili waweze kujiridhidha kumuachia mchezaji huyo, Huku ikielezwa hawana mpango wowote wa kukubali ofa ambayo itachelewa kutoka kwa klabu ya Al Shabab.carrascoAtletico wanahitaji ofa ya mchezaji huyo imwasilishwe mapema klabuni hapo kabla ya siku ya mwisho kufika, Hivo klabu hiyo kutoka nchini Saudua wanapaswa kutuma ofa mapema kabla ya kufika siku ya mwisho ya usajili.

Klabu ya Atletico Madrid imetoa angalizo tayari kwa Al Shabab kua dili hilo litavunjika kama watachelewesha kutuma ofa yao kwajili ya Carrasco,Kinachotakiwa ni Al Shabab waharakishe dili hilo likamilike kwakua klabu imeshakua tayari kumuuza mchezaji huyo.carrascoMchezaji Yannick Carrasco ameshakubaliana maslahi binafsi na klabu ya Al Shabab kilichobaki ni makubaliano baina ya vilabu hivo viwili ili kumruhusu winga huyo wa kimataifa wa Ubelgiji  kukipiga nchini Saudia Arabia siku zijazo.

Acha ujumbe