Beki wa kulia wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Hispania Dani Carvajal anatarajiwa kuukosa mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa wa klabu hiyo ambao watacheza kesho dhidi ya Union Berlin.

Dani Carvajal hajaonekana katika mazoezi ya leo ya klabu ya Real Madrid ambayo ni mazoezi ya mwisho kuelekea kukipiga na Union Berlin katika mchezo wa kesho na taarifa zinaeleza beki huyo amepata majeraha katika mguu wake wa kulia.CarvajalBeki huyo raia wa kimataifa wa Hispania amekua panga pangua kwenye kikosi cha Real Madrid kwa takribani miaka saba sasa, Jambo ambalo linaweza kua kinasababisha majeraha kwa mchezaji huyo kwasasa.

Beki huyo raia wa kimataifa inaelezwa anaweza akaikosa michezo takribani mitatu ukiachana na mchezo wa Union Berlin na michezo hiyo ni dhidi ya Atletico Madrid kwenye Madrid Derby jumapili inayofuata, Las Palmas, na Girona.CarvajalKlabu ya Real Madrid inatarajia kumtumia beki Nacho Fernandez katika upande huo wa kulia au Lucasz Vazquez ambaye nae amekua akitumika katika upande huo pindi beki Dani Carvajal anapokua anakosekana katika michezo ya klabu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa