Kiungo wa timu ya Taifa ya taifa ya Brazil na klabu ya Manchester United Carlos Casemiro amewataka wenzake kua chini na kutulia kuelekea michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Licha ya kuonekana kupewa nafasi kwenye michuano hiyo.casemiroTimu ya taifa ya Brazil ilishinda kombe la dunia miaka 20 iliyopita wakati michuano hiyo ilifanyika Korea kusini na Japan. Wakati huo gwiji wa soka wa Brazil Ronaldo de Lima alimaliza kama mfungaji bora wa michuano hiyo wakati Selecao wakiwa mabingwa wa dunia.

Kiungo huyo wakati anafanyiwa mahojino jijini Manchester amezungumza mambo mengi kuhusu timu yake ya taifa ya Brazil na kufunguka kua anajua kua, Timu yao ya taifa ni miongoni mwa timu za taifa zinazopewa nafasi kubwa kubeba taji hilo.

“Kuna pande mbili katika hilo. Bila shaka, Hakuna cha kujificha kwenye Brazil ni timu pendwa, Lakini sio mara zote wanaopendwa wanashinda katika soka, Wanaopemdwa zaidi sio mabingwa kila wakati” Alisema Casemiro.casemiro“Tunajua kuna timu zingine za taifa zinafanya kazi kubwa, Na timu hizo pia vipenzi, Soka siku hizi linajieleza, Tunajua timu zingine pia zinacheza vizuri sana. Tunajua wajibu wetu, tunatakiwa kuwaheshimu wapinzani wetu tunaokutana nao”Alisema kiungo huyo

Casemiro anaamini licha ya kupewa nafasi kubwa kuelekea michuano lakini bado ametahadharisha kua sio mara zote wanaopewa nafasi wanashinda katika mchezo wa soka.

Timu ya taifa ya Brazil inatarajiwa kuanza kutupa karata yake dhidi ya timu ya taifa ya Serbia tarehe 24 Novemba katika mchezo wa kwanza wa kundi G.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa