Casemiro Amaliza Adhabu Yake

Kiungo wa shoka wa klabu ya Manchester United Carlos Casemiro amefanikiwa kumaliza adhabu yake baada ya kukaa nje ya uwanja katika michezo mitatu ya klabu hiyo.

Mchezo wa mwisho ambao Casemiro ameukosa katika michezo mitatu aliyopewa adhabu ni mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Leicester City ambapo Manchester United wamefanikiwa kushinda mabao matatu katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Old Trafford.CasemiroKlabu ya Manchester United imefanikiwa kucheza michezo yake mitatu ya ligi kuu ya Uingereza bila ya kiungo wake wa shoka, Lakini wamekua na wakati mzuri kwani hawajapoteza mchezo hata mmoja katika michezo hiyo mitatu wakifanikiwa kukusanya alama saba kati ya tisa.

Hofu ilikua kubwa kwa klabu ya Manchester United kucheza bila kiungo Casemiro ambaye alikua ndio mhimili kwenye eneo la katikati kwenye timu hiyo, Lakini Man United licha ya kumkosa mchezaji huyo lakini wameweza kucheza vizuri huku Marcel Sabitzer akionekana kucheza vizuri katika michezo hiyo.CasemiroCarlos Casemiro ni rasmi atarejea katika mchezo wa fainali wa kombe la Carabao dhidi ya klabu ya Newcastle utakaopigwa katika dimba la Wembley siku ya jumapili, Hivo kiungo huyo sasa atakua huru kuwatumikia mashetani wekundu katika kuhakikisha wasaka taji lao la kwanza msimu huu.

Acha ujumbe