Kiungo wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania anakaribia kujiunga na klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza kwa dili litakaloigharimu klabu hiyo kiasi cha euro milioni 60 na nyongeza ya euro milioni kumi.

Nyota huyo wa kibrazil inaelezwa amewaeleza marafiki zake ndani ya Real Madrid kua yuko tayari kujiunga na wababe hao wa zamani nchini uingereza.

Wakati huohuo klabu yake ya sasa Real Madrid watarajiwa kumruhusu kiungo huyo kufanya vipimo vya afya na Man United ndani ya saa 24 zijazo.Taarifa za ndani za klabu ya Real Madrid zinasema ilikua ngumu sana kwa Rais wa klabu hiyo Florentino Perez kukataa ofa waliyopewa na Man United kwa mchezaji huyo aliefikisha umri wa miaka thelathini.

Taarifa za kuaminika zinadai mchezaji huyo ataenda kulipwa karibia mara mbili ya kiasi alichokua akipokea ndani Real Madrid,Pia mkataba mrefu wa miaka minne kukiwa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja kitu kilichomvutia nyota huyo kujiunga na mashetani wekundu.


Mashabiki wa Man United wanahisi huu utakua usajili bora toka kuondoka kwa aliekua kocha wa  klabu hiyo aliepata mafanikio zaidi Sir Alex Ferguson,Kwani  kukosa kiungo asili wa ulinzi ni tatizo lililowasumbua kwa muda mrefu sana na wakati huu wanafikiri wamepata tiba ya eneo hilo,Baada ya kufanikiwa kumpata nyota huyo aliepata mafanikio makubwa ndani Real Madrid.

Carlos Casemiro atakumbukwa kwa matukio mengi ndani ya Real Madrid lakini kubwa zaidi ni kutengeneza utatu mtakatifu katika eneo la kiungo ndani ya Madrid akishirikiana na Toni Kroos pamoja na Luca Modric kuiwezesha club hiyo kubeba mataji manne ya ligi ya mabingwa barani ulaya,La Liga, Spanish Super Cup,Copa de Rey,pamoja na Klabu bingwa  ya dunia.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa